FAHAMU KWANINI PUA ZA WAJAWAZITO HUWA KUBWA KIPINDI CHA UJAUZITO
𝗞𝘄𝗮𝗻𝗶𝗻𝗶 𝗣𝘂𝗮 𝘇𝗮 𝗺𝗮𝗺𝗮 𝗸𝗶𝗷𝗮𝗰𝗵𝗼 𝗵𝘂𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗯𝘄𝗮 ???
Mabadiliko mengi hutokea wakati wa ujauzito, na ‘Pua ya Ujauzito’ ni mojawapo..! Dalili hii isiyozungumziwa sana, inayotrendi kwenye mitandao ya kijamii, inafunua mabadiliko ya kushangaza ambayo wanawake hupitia, katika harakati za kuleta uhai mpya duniani. 🤰✨
Je, wajua? Mwili wako huzalisha damu na maji maji ya ziada kwa asilimia 50 wakati wa ujauzito, hali inayosababisha kuvimba sehemu kadhaa za mwili ikiwemo pua! Hii inaweza kuanza katika trimesta ya pili na kuwa kali zaidi katika ya tatu. Ni sehemu ya maandalizi ya mwili wako kwa ajili ya kujifungua mtoto wako. 🌟
Ingawa kuna machache unayoweza kufanya kudhibiti hili, kumbuka, ni mabadiliko ya kawaida na ya muda.
Kumbatia kipindi hiki kwa upendo, furaha na ucheshi – ni sehemu moja tu ya safari ya ajabu ya umama! ❤️👶 #SafariYaUmama
0684 450 076

Comments
Post a Comment