Faida Za mboga za Majani
:Mboga za Majani huwa na Nyuzinyuzi zinazosaidia kuboresha Mfumo wa Chakula na kutoa Kinga dhidi ya #Saratani ya Utumbo Mkubwa
Pia, huwa na Madini ya Potassium ambayo husaidia kudhibiti Shinikizo Kubwa la Damu na Magonjwa ya Moyo
Soma zaidi nakala za hivi
Hakuna aina moja ya mboga za majani inayotosha kukupatia virutubisho vyote muhimu ili uweze kuimarisha afya yako.
Ni muhimu kutokutumia aina moja ya mboga kila siku kwa kuwa haiwezi kukupatia virutubisho vyote unavyohitaji, bali jitahidi kuchanganya au kubadili mara kwa mara ili uweze kunufaika vizuri.
Mboga za majani huwa na faida zifuatazo kwa afya-
Huwa na nyuzinyuzi zinazosaidia kuboresha mfumo wa chakula, kurahisisha choo na kutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo mkubwa
Aina nyingi za mboga za majani huwa na madini ya potassium ambayo husaidia kudhibiti shinikizo kubwa la damu na magonjwa ya moyo
Huwa na kipimo kidogo cha sukari (Low Glycemic Index) hivyo hufaa sana kwa watu wenye tatizo la ugonjwa wa kisukari
Kama ilivyo kwa makundi mengine ya chakula, mboga za majani hubeba virutubisho muhimu kwa afya yako kama vile vitamini A, vitamini C, asidi ya foliki, madini mbalimbali na viondoa sumu. Vyote hivi huhitajika mwilini ili kujenga afya.
Comments
Post a Comment