JINSI YA KUPIKA MBOGA ZA MAJANI KUPATA VIRUTUBISHI VYAKE NA FAIDA ZAKE
FAHAMU:NAMNA YA KUPIKA MBOGA ZA MAJANI
Watu wanakula mboga za majani kwa lengo la kupata kiburudisho na wengine ili siku iende tuu.
Wengi wanakosea kupika mboga za majani ili kupata virutubisho kama vitamins na madini chuma
Zingatia haya ukiwa unapika mboga
1.Osha mboga za majani kwa maji safi kabla ya kuzikatakata.
Kamwe usioshe baada ya kuzikatakata
2. Pika kwa muda mchache.
Virutubisho vyake ni heat labile; ukichemsha sana vinaharibika.
3. Pika ukiwa umefunika kwa mfuniko. Kuacha wazi kutapoteza virutubisho
4. Usipike chukuchuku (bila mafuta); virutubisho vinavyopatikana kwenye mbogamboga vinahitaji kiasi cha mafuta ili kimeng'enywe na kuingia kwenye mfumo wa damu wa mlaji.
Hivyo, ukila bila kuweka mafuta, unapoteza virutubisho vingi.
Weka mafuta salama kwa mlaji hata kijiko kimoja tu.
Gusa hapa chati nami
FAIDA ZA KULA MBOGA ZA MAJANI
1. Kupata virutubisho muhimu kama vitamins ili kusaidia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili na mfumo wa fahamu (Vitamin B12)
2. Kupata virutubisho kusaidia kuongeza damu.
3. Kusaidia kupata nyuzinyuzi (fibres) kuepuka choo kigumu (constipation)
Comments
Post a Comment