SABABU ZA SHINGO KUKAZA NA KUUMA

LEO tutaangazia maumivu ya shingo tatizo ambalo watu wengi nchini limewahi kuwapata katika maisha yao ya kila siku. Tatizo hilo huwa na maumivu ya wastani mpaka makali yasiyovumilika. Ukiizungumzia shingo kisayansi ni kwamba kwa ujumla imeundwa na pingili za vifupa vidogo vilivyoanzia katika fuvu la kichwa. Katika ya vifupa hivyo huwa na pingili kama santuri plastiki kitaalamu huitwa cervical disc ambazo hukaa kati ya pingili moja na nyingine kazi yake ni kunyonya shinikizo la uzito na kuzuia msagiko. Vifupa, nyuzi ngumu za ligamenti na misuli ya shingo kazi yake ni kutoa msaada kwa kichwa na kuwezesha miendo mbalimbali ikiwamo pembeni na kujizungusha. Hivyo basi hitilafu yoyote, shambulizi au majeraha yakitokea ya aina yoyote yakitokea yanaweza kusababisha maumivu makali ya shingo. Chanzo kikubwa cha kujitokeza kwa tatizo hili ni kujeruhiwa kwa misuli ya shingo pale unapokuwa umelala vibaya kama vile wakati wakulala usiku, wakati wa kucheza au mazoezi, kut...