Dalili za Pumu

 Ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa upumuaji baada ya njia ya kupitishia hewa (bronchieal tube) kuvimba na kutengeneza Ute (mucus) ambayo kupelekea njia ya hewa kuwa ndogo, mgonjwa huanza kupata shida ya Kupumua, kukohoa, kutoa sauti Kama filimbi na wengine Kushindwa kuongea.


Asthma/Pumu huwapata Rika na jinsia zote wakubwa kwa Watoto.


Pumu haina chanzo mahususi (halisi), bali hufananishwa na kulinganishwa na mazingira flani.


Dalili za Pumu 

Mgonjwa wa pumu huonyesha dalili kadha wa kadha Kati ya hizo ni hizi zifatazo.


Kupata shida ya Kupumua


Kifua kubana na kifua kuuma


Kukoh/kikohozi


Kutoa sauti kama filimbi wakati wa kutoa hutoa hewa.


Kushindwa kulala/kupata shida wakati wa kulala kwa sababu ya Kushindwa Kupumua vizuri.


Wakati mwingine Pumu hutokea/huamshwa na mazingira flani ya nje au Hali ya hewa.


Shughuli katika mazingira flani - Baadhi ya watu hupata tatizo la Pumu kwa sababu ya kazi hujulikana Kama (exercises induced asthma) mfano wanaofanya mazingira yenye baridi sana, na  hewa kavu.


Mzio (Aleji) - watu wengine huamsha Pumu kwa sababu ya mzio au Aleji (allergies induced asthma)) ya vitu mfano vumbi,


Kazi - kundi lingine la watu wengine hupapata asthma kwa sababu ya kazi wanazo fanya (occupation asthma) mfano wakulima wanaopulizia dawa mashambani,viwanda vya gesi na kazi zinazohusisha vumbi, moshi


Mazingira ambayo yanaweza kuamsha/kusababisha tatizo la Pumu ni pamoja.


Chanzo Cha Pumu/Asthma

Pumu haisababishwi na kitu kimoja huweza kusababishwa na vitu vingi,


Mzio/Aleji ya vumbi,moshi,


Kurithi kutoka kwenye familia ambayo ina watu au mtu mwenye Pumu.


Mazingira ya kazi mfano, kazi za kupulizia dawa shambani, viwandani Kama vya simenti, gesi, makaa,n.k


Uvutaji wa sigara


Kuwa na Uzito au unene kupita kiasi


Msongo wa mawazo


Kiungulia Cha muda mrefu


VIPIMO

Asthma/Pumu huweza kuonekana kwa dalili moja kwa moja lakini, baadhi ya vipimo hufanyika kutofautisha na Matatizo mengine yanyoendana na asthma. Baadhi ya vipimo hivyo ni pamoja na…


Sperometry


Allegly testing


Imaging test eg. Chest x-ray na CT scan n.k


MATIBABU 

Pumu Ni ugonjwa wa kudumu na matibabu yake Ni changamoto mara nyingi kumfanya mhanga kutumia dawa hizo kwa muda wote wa maisha yake.


Mgonjwa atashauriwa kutumia dawa za kusaidia 


Kuondoa uvimbe na kupunguza Ute(mucus) kwenye njia ya hewa kwa njia kumeza vidonge, kuchoma sindano, kuvuta kwa mdomo dawa maalum.


Dawa za kuondoa mzio/Aleji


NAMNA YA KUZUIA

Pumu huweza kuepukika/kuzuilika kutokana na chanzo au kisababishi Cha Tatizo.


Watu wanaoishi au kufanya kazi maeneo yenye vumbi,moshi wanashauriwa kuvaa vifaa vya kuzuia Moshi au vumbi kuvuta wawapo kazini au maeneo yenye vyanzo vya tatizo.


Acha kutumia sigara


Tumia dawa kwa usahihi kwa muda sahihi Kama ulivyo elekezwa na mtaalamu wa afya.


Vaa nguo nzito zenye kutengeneza joto kuepuka kuacha kifua wazi kipindi/Maeneo ya baridi kali.


Tibu tatizo la mafua 


Epuka tatizo kiungulia 


Fanya mazoezi ya mwili kuweka afya vizuri 


Epuka Uzito na Unene uliokithiri


Tofauti na zamani Sasa asthma inatibika kwa tiba mbadala kwa njia ya Mimea na matunda. Tuna Virutubisho bora vinavyoweza kuzuia tatizo na kuondoa tatizo la Pumu kwa Umri wote.


Karibu tukuhudumie kuondoa changamoto ya tatizo la Pumu/Asthma.

Kwa Maoni | Ushauri | Matibabu

Tupigie Sasa / Tuma SMS


0684450076


Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU SIRI ZA DAWA ZA VIDONDA VYA TUMBO

NMN KUTIBU SUKARI,PRESHA,TEZI DUME NA NI ANT_AGING

JINSI YA KUPIKA MBOGA ZA MAJANI KUPATA VIRUTUBISHI VYAKE NA FAIDA ZAKE