UJUWE UGONJWA WA TEZI DUME NA LISHE KUJIKINGA


 #Tezidumenini


IJUE TEZI DUME NI NINI DALILI MADHARA NA TIBA YAKE BILA UPASUAJI


Tezi dume ni moja ya tezi ya uzazi ya kiume ambayo kila mwanaume anayo, tezi hii lipo chini ya kibofu cha mkojo na inazunguka njia ya mkojo toka kwenye kibofu kwenda kwenye uume.


*NOTE:Jinsi umri unavyoongezeka tezi dume nayo huongezeka ukubwa ambao unaweza kuwa wa kawaida au Saratani.*


Kuna aina tatu za magonjwa ya tezi dume.

•Maambukizi ya Bakteria (Prostatitis).


•Kukua kwa tezi dume ambayo sio Saratani (Benign Prostatic 

Hypertrophy-BPH).


•Saratani ya tezi dume.


*KAZI YA TEZI DUME*


•Kutoa majimaji anayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) kutengeneza manii (semen).


*SARATANI YA TEZI DUME*


Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vitokanavyo na saratani kwa wanaume duniani.


Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 40 na kuendelea.


*VISABABISHI VYA SARATANI YA TEZI DUME*


Chanzo hasa cha saratani ya tezi dume hakijulikani, saratani hii ina uhusiano mkubwa na;


•Umri, Wanaume wenye umri kuanzia 

miaka 40 na kuendelea wanapata zaidi saratani ya tezi dume.


•Vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta, hasa ya wanyama.


•Historia ya tatizo hili kwenye familia (Genetic).


•Kuwa na uzito uliokithiri.


*DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME*


Katika hatua za awali, dalili hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume Isiyokuwa Saratani (BPH).

Dalili hizo ni pamoja na; 


•Kusikia kupata haja ndogo mara kwa mara hasa nyakati za usiku.


•Haja ndogo kuchelewa kutoka unapoanza kukojoa.


•Kutoa mkojo wenye mtiririko dhaifu na kuchuruzika kidogo kidogo baada ya kumaliza kukojoa. 


•Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote.


•Kutoa mkojo au manii 

yaliyochanganyika na damu.


•Maumivu makali sehemu mbalimbali za mwili kama Saratani imesambaa.


•Kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu na kizunguzungu.


*UCHUNGUZI / UPIMAJI*

•Uchunguzi kwa kutumia kidole cha shahada kupitia njia ya haja kubwa na kuhisi ukubwa wa tezi kwenye ukuta wa puru.


•Kipimo cha damu kuangalia kiwango cha aina ya ‘protein’ iitwayo ‘Prostate 

Specific Antigen (PSA), proten’ hii huwa juu kuliko kawaida kama mtu ana Saratani ya Tezi  Dume na wakati mwingine kama ana maambukizi (prostatitis).


•Kuchukua kipande cha nyama kwenye tezi (Prostate Biopsy) kwa uchunguzi wa kimaabara.


•Kipimo cha mawimbi sauti (Ultrasound) ambacho husaidia kuonyesha ukubwa na sura ya tezi dume.


•Vipimo vya CT scan, MRI kutambua kama Saratani imesambaa sehemu nyingine za mwili.


*TIBA YA UVIMBE TEZI DUME IPO KWA NJIA YA ASILI BILA UPASUAJI :


TUWASILIANE kwa msaada zaid ushaur ni bure kabisa


0684450076


#ugonjwawatezidume

#dalilizatezidume

#madharayatezidume

#tibayatezidume

#tezidume

#ProstateRelax


Gusa links watsapp

Comments

Popular posts from this blog

FAHAMU SIRI ZA DAWA ZA VIDONDA VYA TUMBO

NMN KUTIBU SUKARI,PRESHA,TEZI DUME NA NI ANT_AGING

JINSI YA KUPIKA MBOGA ZA MAJANI KUPATA VIRUTUBISHI VYAKE NA FAIDA ZAKE