UFANYE NINI UKIWA UNAPATA MAUMIVU KWENYE KUNYONYESHA FAHAMU
Ufanye nini unapopata maumivu ya maziwa wakati wa kunyonyesha?
Mara kadhaa wanawake wanaonyonyesha hupata maumivu ya maziwa. Hali hiyo inaambatana na ziwa kuvimba na kuwa jekundu. Tatizo hilo husababishwa na kuziba kwa mirija midogo inayosafirisha maziwa kupeleka kwenye chuchu. Maambukizi ya bakteria hufuatia baada ya mirija kuziba.
Dalili
•Kuhisi maumivu kama ziwa linawaka moto
•Ziwa kuvimba na kuwa na ugumu
•Kupata maumivu wakati wa kunyonyesha
•Wakati mwingine mama anapata homa,
Matibabu
Iwapo mama amepata tatizo hili anahitaji kufanya mambo yafuatayo kama sehemu ya matibabu
•Pata muda wa kutosha kupumzika.
•Tumia vinywaji au vyakula vyenye majimaji kwa wingi
•Nyonyesha mtoto mara nyingi uwezavyo mfano kila baada ya saa 2-3. Mama anaponyonyesha itamsaidia kuondoa maambukizi na pia ni salama kwa mtoto. Mdomo wa mtoto unapaswa kufunguka sana, na chuchu yote ingizwe ndani ya mdomo wa mtoto.
•Anza kunyonyesha upande wenye maumivu, ili mtoto aweze kumaliza maziwa yote kabla hajashiba.
•Kanda ziwa taratibu kwa kutumia kitambaa safi na maji ya vuguvugu.
•Iwapo mama anapata homa anahitaji kutumia dawa
0684450076
#Share na marafiki wajifunze pia
watsapp
Comments
Post a Comment