SABABU ZA SHINGO KUKAZA NA KUUMA
LEO tutaangazia maumivu ya shingo tatizo ambalo watu wengi nchini limewahi kuwapata katika maisha yao ya kila siku.
Tatizo hilo huwa na maumivu ya wastani mpaka makali yasiyovumilika.
Ukiizungumzia shingo kisayansi ni kwamba kwa ujumla imeundwa na pingili za vifupa vidogo vilivyoanzia katika fuvu la kichwa.
Katika ya vifupa hivyo huwa na pingili kama santuri plastiki kitaalamu huitwa cervical disc ambazo hukaa kati ya pingili moja na nyingine kazi yake ni kunyonya shinikizo la uzito na kuzuia msagiko.
Vifupa, nyuzi ngumu za ligamenti na misuli ya shingo kazi yake ni kutoa msaada kwa kichwa na kuwezesha miendo mbalimbali ikiwamo pembeni na kujizungusha.
Hivyo basi hitilafu yoyote, shambulizi au majeraha yakitokea ya aina yoyote yakitokea yanaweza kusababisha maumivu makali ya shingo.
Chanzo kikubwa cha kujitokeza kwa tatizo hili ni kujeruhiwa kwa misuli ya shingo pale unapokuwa umelala vibaya kama vile wakati wakulala usiku, wakati wa kucheza au mazoezi, kutumia kompyuta muda mrefu au kukaa katika viti vya kwenye gari, ofisini na nyumbani.
Pia tatizo hili linaweza likawa ni shambulizi la mifupa pingili za shingo kutokana na kutumika na kulika kwa mifupa hiyo, mgonjwa kuwahi kupata ajali iliyomuumiza shingo, kupata magonjwa ya shingo na matatizo ya mishipa ya fahamu hasa ya shingoni.
Hutokea mara chache kwa baadhi ya watu wenye dalili ya maumivu ya shingo likawa ni tatizo kubwa, mara nyingi huwa ni maumivu ya kawaida tu yanayoweza kuisha kwa siku chache. Kwa kawaida maumivu ya kawaida ya shingo huwa yanaweza kuchukua siku mbili hadi tano yakapotea yenyewe. Maumivu haya huwa ni kero na yanaweza kuwa makali na hatari kwa sababu shingo inapitisha mamia ya mishipa ya fahamu ndio maana huwapo na hisia kali za maumivu iwapo shingo inauma.
Hivyo kama unasumbuka na maumivu makali na ya muda mrefu unaweza muona daktari kwa uchunguzi ama wasiliana mimi sasa nikushauri
0684 450 076
Comments
Post a Comment