Dalili za Pumu

Ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa upumuaji baada ya njia ya kupitishia hewa (bronchieal tube) kuvimba na kutengeneza Ute (mucus) ambayo kupelekea njia ya hewa kuwa ndogo, mgonjwa huanza kupata shida ya Kupumua, kukohoa, kutoa sauti Kama filimbi na wengine Kushindwa kuongea. Asthma/Pumu huwapata Rika na jinsia zote wakubwa kwa Watoto. Pumu haina chanzo mahususi (halisi), bali hufananishwa na kulinganishwa na mazingira flani. Dalili za Pumu Mgonjwa wa pumu huonyesha dalili kadha wa kadha Kati ya hizo ni hizi zifatazo. Kupata shida ya Kupumua Kifua kubana na kifua kuuma Kukoh/kikohozi Kutoa sauti kama filimbi wakati wa kutoa hutoa hewa. Kushindwa kulala/kupata shida wakati wa kulala kwa sababu ya Kushindwa Kupumua vizuri. Wakati mwingine Pumu hutokea/huamshwa na mazingira flani ya nje au Hali ya hewa. Shughuli katika mazingira flani - Baadhi ya watu hupata tatizo la Pumu kwa sababu ya kazi hujulikana Kama (exercises induced asthma) mfano wanaofanya mazingira yenye baridi sana, na...